Loading...

Maisha Ni Safari - Lesson 1

Wongofu

Kuangalia nyuma kuhusu uzoefu wako wa wongofu. Mara nyingi ni wazo nzuri ya kuangalia nyuma kuhusu uzoefu wako wa wongofu. Je, ni nini kilichotokea  wakati ulifanyika mfuasi wa Yesu Kristo? Je, wewe ulifahamu jambo lolote? Je, kuna uwezekano wa kuwa haukuelewa chochote? Je, kuna kitu chochote kulichotokea ambacho unaweza kuwa ulikifahamu?

Bill Mounce
Maisha Ni Safari
Lesson 1
Watching Now
Wongofu

Lessons
About
Resources
  • Kuangalia nyuma kuhusu uzoefu wako wa wongofu. Mara nyingi ni wazo nzuri ya kuangalia nyuma kuhusu uzoefu wako wa wongofu. Je, ni nini kilichotokea  wakati ulifanyika mfuasi wa Yesu Kristo? Je, wewe ulifahamu jambo lolote? Je, kuna uwezekano wa kuwa haukuelewa chochote? Je, kuna kitu chochote kulichotokea ambacho unaweza kuwa ulikifahamu?

  • Mabadiliko yale yanayotokea katika maisha yako. "Wongofu" ni kumaanisha kuwa kwa jambo moja hadi jingine. Katika hali yako, wewe ulibandilika kutoka  kutokuwa mwanafunzi wa Yesu hadi kuwa mmoja. Pia ina maanisha kwamba Mungu anafanya kazi sasa katika maisha yako, kwa kuanzia na kukufanya wewe uwe kama Yesu. Je, unastaajabu kuhusu jambo hili? Ni nini hasa kilichotokea wakati ulifanyika Mkristo? Je haya maisha mapya kama mfuasi wa Yesu yako vipi? Je, maisha yangu yalibadilika moja kwa moja?

  • Wakati unapojikwa katika matebezi yako mapya na Mungu. Hata kama nguvu za Mungu zinafanya kazi ndani yako, kukusaidia kuwa zaidi kama Yesu, unaweza kujikwa. Hii haifai kuondoa furaha ya imani yako mpya; ni ya kukuandaa kwa ajili ya furaha ya ukuaji wa kiroho ilio mbele. Mungu anaifahamu na siyo ya kushangaza, na haiathiri ahadi yake kwetu. "Dhambi" ni nini? Je; majaribu ya dhambi? Wawezaje kumwambia Mungu kwamba ulitenda dhabi na unaomba msamaha? Je, yeye husamehe? Je, unaweza kusafishwa?

  • Kipengele muhimu ya uhusiano wowote ni mawasiliano, wote kusikiliza na kuzungumza. Mungu alisema na sisi njia mbili za msingi, kwa kuunda na kupitia Neno lake, Biblia. Je, maneno "msukumo," "mamlaka," na "mpangilio" yanamaanisha nini? Je, tunaweza kuamini Biblia? Je, naweza kumsikiliza Mungu wakati ninasoma maneno yake? Mimi ninatakiwa kufanya kitu chochote zaidi ya kuisoma?

  • Mawasiliano bora  inahitaji siyo tu kusikiliza lakini pia kuzungumza. Maombi ni kuzungumza na Mungu, kuhusu chochote na kila kitu. Yeye ni Baba yetu mpya, na anataka kusikia kutoka kwetu. Jinsi gani unaweza kuomba? Je, kuomba juu ya nini? Na kama mimi nina shida kumsikiliza akiongea?

  • Wakati ulifanyika Mkristo, ulielewa mambo fulani kuhusu Mungu. Lakini unajua kwamba anajua kila kitu? Kuwa yeye yuko kila mahali? Kuwa yeye ni mwenye nguvu zote? Ni jinsi gani basi tunapaswa kukabiliana na maarifa kamili ya Mungu? Ibada ni nini? Je, tunapaswa kujibu vipi kwa yale tunajua kuhusu Mungu?

  • Yesu ni mtu anayejulikana katika historia. Yeye ameathiri historia ya dunia kuliko kiongozi yeyote mwingine au filosofia au harakati za kisiasa. Watu wengi hujua jina, lakini yeye ni nani? Alisema nini kuhusu yeye mwenyewe? Je, wafuasi wake walisema nini juu yake? Je; umuhimu na sababu kuhusu maswali haya na majibu yetu ni nini?

  • Yesu alifanya mambo mengi alipokuwa duniani, lakini muhimu zaidi ya yote alikuwa afe msalabani. Lakini nini hasa kilichotokea? Ni nini iliokamilika? Biblia inamaanisha nini wakati inazungumza juu ya Yesu kuwa "Mwana kondoo wa Mungu"? Je, kuna kitu chochote ambacho kinaweza kunisaidia kuelewa umuhimu wa kifo chake. Je, kuna haja kukumbushwa kuhusu suala hilo mara kwa mara?

  • Wakristo wanaamini Mungu Mmoja; tunaamini katika Mungu mmoja. Lakini pia ni Utatu; tunaamini katika "utu" ya Utatu - Mungu Baba, Mungu Mwana, na Mungu Roho Mtakatifu. Ni nani huyu ambaye ni mwanachama wa utu wa Utatu? Ni nini hasa kazi yake? Jukumu lake inayoendelea katika maisha yangu ni nini? Ina maana gani kuongozwa na kuwezeshwa na Roho Mtakatifu? Je ninahitaji kufanya kitu chochote, au yeye hufanya kazi yote? Tungekuwa wapi kama si kwa kazi ya Roho Mtakatifu?

  • Wakati ulipofanyika Mkristo, wewe ulianza kutembea na Mungu. Ni mchakato wa  siku-kwa-siku ambao dhambi haina mamlaka juu ya maisha yako na unabadilika kuwa kama Yesu. Lakini baadhi ya siku ni ngumu kuliko zingine, hasa wakati mambo magumu yanapotokea. Kwa nini haya "mambo mabaya" hutokea? Naweza kujiwekea sehemu yangu mwenyewe kutoka kwa Mungu ikiwa kufanya hivyo kutanisaidia kuepuka maumivu? Je, kuna madhara yoyote kwa kuruhusu dhambi katika baadhi ya maeneo ya maisha yangu? Ina maana gani kwamba Yesu ni "Mwokozi" na "Bwana"?

  • Wakati tumekuwa watoto wa Mungu mwanafunzi mmoja kwa wakati, kama watoto sisi ni watu wa familia mpya na baba mpya, ndugu wapya na dada, na nyumba mpya. Je, mimi kuhusiana na watu hawa? Je, mimi ninahaja ya kutumia muda pamoja nao? Je, hii ni kazi rahisi au gumu? Ni kwa jinsi gani kanisa la kwanza kutusaidia kuelewa masuala haya? Ni kwa jinsi gani upendo wangu kwa Mungu huonyesha yenyewe kwa wengine?

  • Wanafunzi wanafaa kufanya wanafunzi zaidi. Hii ni moja ya uzoefu wenye furaha zaidi katika maisha yako unaposhiliki jinsi Mungu amekupa uzima, na atawafanyia hivyo rafiki zako, majirani, na wengine. Huu sio mchakato wa kutisha; ni asili kwa watu ambao wamebadilishwa na wanaishi maisha mapya.  Je; watu watakujibu namna gani? Je "ushuhuda binafsi" ni nini? Je, jinsi gani naweza kuwaambia watu  kwamba wao pia wanaweza kuwa manafunzi wa Yesu? Nini kama wao si kama mimi?

English | Hindi | Swahili | Spanish | Arabic

Mtaala wetu wa wiki 12 unaongoza wanafunzi katika mwelekeo sahihi na kuhamasisha waumini waliokomaa kuwashauri. Katika wiki ya kawaida, mwanafunzi anahusika na maandiko ya Biblia na kupata moyo wa kuanza safari, kuomba na kukariri mistari ya kibiblia. Kisha mwanafunzi na mshauri wanasikiliza dakika thelathini za majadiliano ya maelezo kuhusu utafiti iliotolewa, kasha wafanye kazi kupitia maswali ya kutafakari kwa pamoja na kisha wawe na siku mbili zaidi kuonyesha kile walichojifunza. (7:40)

Downloads